DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, March 26, 2014

SIFANYI FILAMU KUUZA SURA – Q CHILLAH



 

Chillah amewataka watu na wadau mbalimbali kutambua kuwa kufanya kwake filamu sio kwa lengo la kuuza sura au kukimbia majukumu yake ya muziki.

Chillah amesema kuna watu wanaodhani uamuzi wake wa kufanya filamu umetokana na kushindwa kufanya muziki.
“Hakuna kinachoshindikana katika maisha,” ameiambia Bongo5. “Kama kuna watu muhimu wananiambia nifanye filamu nitaendelea kufanya. JB na Adam Kuambiana Director waliniambia kuna filamu ya kufanya ‘Hukumu Ya Ndoa Yangu’ na bado JB aliambia niwe kwenye kampuni yake Jerusalem ili tufanye mambo makubwa zaidi ila nikamwambia bado kwanza kwa sasa. Japokuwa mimi si mtu wa filamu watu wengi wanapenda nifanye filamu. Kwahiyo nashangaa baadhi ya watu wanadhani nimeenda kwenye filamu kwaajili ya kuuza sura na kukimbia majukumu yangu ya muziki. Jamani mimi ni msanii Mkubwa sana na nina uwezo mzuri wa kuimba na kufanya vitu vizuri sana katika muziki. Kwahiyo nitaendelea kufanya muziki wangu mzuri na kama nitahitajika kufanya filamu nitafanya.Lakini maisha yangu nyuma ya pazia naweza sana kufanya filamu vizuri sana,na pia si biashara.”


No comments: