DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, September 25, 2013

Mke wa 2Face mjamzito


 
Mke wa mwanamuziki 2 Face Idibia, Annie Macaulay amethibitika kuwa ni mjamzito kwa sasa na anatarajia katika siku za usoni kujifungua mtoto ambaye atakuwa ni wa 7 wa msanii huyu ambaye amejijengea heshima kubwa Afrika na duniani kwa kipaji kikubwa cha kuimba.

Tayari tumbo la bibie Annie limekwishaonyesha dalili zote za ujauzito kama alivyoonekana hivi karibuni huko Abuja, na ndani ya familia hii rasmi ya msanii huyu, mtoto atakayezaliwa atakuwa wa pili.

Kama ambavyo inafahamika, Msanii huyu ana watoto wengine watano kutoka katika mama tofauti nnje ya familia yake rasmi, Watoto ambao ni dalili tosha kuwa msanii huyu ni mtu wa familia.

No comments: