DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, September 26, 2013

Wakazi kujiweka poa Bongo

 


Rapa Wakazi ambaye anafanya poa sana katika game ya rap bongo huku ikiwa inaaminika kuwa asilimia kubwa ya mashabiki na wapenzi wa muziki wake wanatokea nnje ya mipaka ya nnchi, ameweka wazi sababu ya muziki wake kueleweka sana ugenini tofauti na hapa Tanzania ambapo ndipo chimbuko lake.

Wakazi amesema kuwa, kukubalika zaidi nnje ya nnchi kumetokana na yeye kukaa na kufanya muziki huko kwa muda, ambapo kwa asilimia kubwa watu wengi wamekuwa wakifuatilia kazi zake kwa njia ya mtandao ambao hapa Tanzania bado unatumiwa na asilimia chache ya watu.

Wakazi pia amewataka Mashabiki wake kukaa tayari kwa Onyesho kubwa la utambulisho wake ambalo litafanyika hivi karibuni sambamba na uzinduzi wa video yake kali ya ngoma inayofahamika kama Touch ambayo ameifanya huko Afrika Kusini.

No comments: