
Msanii anayefanya poa sana sasa hivi kwenye mziki wa Bongo fleva kwa kuiwakilisha vyea Tzee nje ya nchi, Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa, amefunguka juu ya chanzo cha kuandika ngoma yake mpya ya ‘Chereko Chereko’ kupitia akaunti yake ya Facebook.
“Ngoma ya “Mganda” ndio ilini-inspire kufanya “Chereko Chereko” lakini baada ya kuingia Studio..the rest is History.I always wanted to do something for my country..sio unyamwezi kila siku! I am proud of what i did,proud of my country,my people and our cultures!” – Ameandika Cpwaa kwenye akaunti yake.
Mganda ni ngoma ya kabila la Kingoni, kabila linalopatikana kusini mwa Tanzania. Ngoma hiyo huchezwa na wanaume watupu wakiwa wamevalia mashati meupe, kaptula nyeupe, mkanda mweusi, soksi nyeupe, viatu vyeusi vilivyong’arishwa vizuri na mara moja moja kofia nyeupe kichwani. Mkononi lazima uwe na usinga mweusi. Ala zitumikazo ni filimbi kwa kila mchezaji na ngoma moja.
No comments:
Post a Comment