
Msanii wa muziki wa Dancehall anayefanya poa sana kutoka Kenya, Redsan ameingia katika changamoto kubwa ya kiushindani kwa sasa hasa baada ya kushambuliwa kwa diss kali kutoka kwa wasanii wanaofahamika kama The New School Kings Of Dancehall.
Hatua hii imehesabiwa kama moja ya njia ambayo jamaa wameamua kutumia kumuonyesha Redsan kuwa wakati wake wa utawala katika muziki wa Dancehall umekwishapita na wao wanakuja kuleta ladha mpya.
Kundi hili ambalo linaundwa na wasanii watatu limeamua kutoa riddim ambayo tayari wamekwishatoa na video yake ikiwa ni mashambulizi yanayoelekezwa kwa Redsan, na sasa mitaa inasubiri kuona ni kwa namna gani staa huyu atajibu mashambulizi.
No comments:
Post a Comment