
Msanii wa muziki wa nchini Kenya, Rufftone amepata shavu kutoka ubalozi wa Korea nchini huko ambapo kuanzia sasa atakuwa ni Balozi wa Mahusiano Mema wa nchi hiyo ndani ya Kenya.
Sambamba na shavu hili kubwa, Rufftone pia amepatiwa cheti ambacho kinathibitisha nafasi yake hii ambayo inaongeza heshima na hatua katika maendeleo yake kama msanii na kama kioo cha jamii.
Rufftone amedhihirisha furaha kubwa aliyonayo kwa kupata nafasi hii na ametoa shukrani zake kwa Mungu pamoja na kila ambaye amekuwa akimsapoti katika kazi zake ambazo zimekuwa zikishuhudia mafanikio siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment