
Tamasha kubwa la burudani linalofanyika kila mwaka likiwa na jina kubwa ‘FIESTA’ safari hii likiwa limepewa udhamini wa nguvu kutoka Serengeti Breweries Limited kupitia bia ya Serengeti, limevunja rekodi ya kuwa tamasha kubwa zaidi kuwahi kufanyika ndani ya Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Tamasha la Fiesta mwaka huu lilijumuisha mikoa 14 ambapo kwa mara ya kwanza ilihusisha mikoa ya Kigoma, Mwanza na Zanzibar huku semina za fursa zikizidi kuipa heshima tamasha hilo na kulifanya la tofauti zaidi lisilowahi kutokea duniani. Pia lilihusisha utolewaji wa zawadi kwa watu mbalimbali mikoani kama vile Pikipiki n.k.






Shukrani na pongezi za kipekee ziende kwa uongozi mzima wa Clods Fm na kila aliyeshiriki kufanikisha tamasha hilo ikiwemo kampuni ya bia Tanzania Serengeti Breweries Ltd.
No comments:
Post a Comment