DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, October 25, 2013

Nisher kuibua vipaji











 


Katika kujaribu kusaidia wasanii wachanga kutimiza ndoto zao katika tasnia ya filamu, na pia kutoa nafasi ya vipaji vya uigizaji ambavyo vimekosa nafasi kuonyesha kile wawezacho, Msanii mahiri wa filamu Bongo, Nisha Jabu amesema kuwa yeye kupitia kampuni yake ya utayarishaji filamu watakuwa wakifanya usahili mara kwa mara kama njia moja wapo ya kuwaibua wasanii hawa chipukizi katika fani hiyo.

Nisha amesema kuwa katika kila kazi mpya ambayo kampuni yake itafanya, basi hiyo itakuwa ni nafasi pia ambayo atatumia kufanya usahili kupata vipaji vichanga  ambavyo atavitumia katika kazi zake hizi na hivyo kuwapatia nafasi ya kuonekana.

Msanii huyu katika mahojiano tuliyofanya naye amesema kuwa anawapenda sana wasanii chipukizi na anafahamu ni kwa jinsi gani wanahangaika kila siku kutafuta njia ya kutokea kupitia sanaa hiyo sababu pia haya yeye alisota sana kabla ya mambo yake kumnyookea katika uigizaji mpaka sasa anamiliki kampuni yake mwenyewe ya utayarishaji filamu.

Muingizaji huyo huyu amewataka wapenzi wa filamu kutarajia kuona mambo mapya na vipaji vipya kabisa na vikali ambavyo pia tayari amekwishaanza kuvitumia katika kazi zake ambazo zitakuwa zinatoka kuanzia sasa.

No comments: