
Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa ngoma yoyote wala kushirikishwa na msanii yoyote kutokana na kujihusisha na sanaa kwa upande mwingine, Buffgzinga ambaye hapo awali alikuwa akijulikana kwa jina la Buff G kiraka kutoka East Coast Team ameamua kurudi tena kwenye gemu la mziki huu ambao anaudai.
Wimbo huo ambao bado haujaachiwa rasmi wamepewa shavu watu watatu; G Nako, Alinda na Snare , unakwenda kwa jina la Bizz Show.
“Sio kwamba niliacha kufanya mziki kabisa ila kuna watu ambao wameonekana sana kwenye huu mziki bilam watu kujua kuwa kuna mengi nilikuwa nayafanya nyuma yao ili kuhakikishakila kitu kinakuwa poa mbele yao. Kikubwa ni kwamba watu wasikilize kile nilichokifanya humu ndani nina uhakika sijawaangusha maana sio kawaida yangu kuwaangusha. Tupo pamoja.” – Buffgzinga.
No comments:
Post a Comment