DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, November 14, 2013

Baby Madaha kukwea pipa

 
Baby Madaha, msanii wa muziki ambaye ana harakati kibao katika nafasi yake kama msanii na kioo cha jamii, anatarajia kukwea pipa kwenda kupiga shoo huko jijini London nchini Uingereza mwishoni mwa mwezi huu.

Msanii huyu ambaye hivi karibuni alizindua video yake mpya inayokwenda kwa jina Squeeze Me Tight kupitia shoo kali ya Friday Night Live ya EATV, kwa mujibu wa Meneja wake Mr Kariuki Joe, anatarajia kuwarusha vilivyo wapenzi wa muziki wake nchini humo katika onyesho ambalo pia litaambatana na uzinduzi wa bidhaa za urembo ambazo ni brand yake mwenyewe.

Msanii huyu ambaye kwa sasa anasimamiwa kazi zake za muziki chini la lebo ya Candy and Candy ya huko Jijini Nairobi, ameonyesha kasi ya ajabu katika gemu hasa baada ya kuanza kufanyakazi na lebo hii, dalili ambayo inaashiria kuwa katika siku za usoni atakua ni nyota ambayo inatisha Afrika kimuziki.

No comments: