
Mbali na kazi hii, Dalilah amesema kuwa anawafagilia sana madiva wanaofanya muziki wa aina hiyo huku akimwagia sifa kemkem mwanadada Lady Jaydee pamoja na K-Lynn akisema kuwa ni wasanii ambao amekuwa akiwafuatilia kwa karibu na kupenda aina ya muziki wanaoufanya.
Msanii huyu amesema kuwa kazi hii ni mwanzo tu wa mambo mazuri kutoka kwake ambapo amewaomba mashabiki kukaa tayari kwa mfululizo wa kazi nzuri kutoka kwake.
No comments:
Post a Comment