
Rapa Jocelyn Tracy, maarufu zaidi kwa jina Keko ameamua kuhamia huko Afrika Kusini kuendeleza mishe zake za muziki, sababu kubwa ikitajwa kuwa ni kutafuta nafasi ya kuufanya muziki wake uwe ni wa kimataifa zaidi.
Mkataba ambao msanii huyu alisaini na kampuni ya maarufu ya kimataifa ya kusimamia kazi za wasanii duniani nyenye makao makuu yake huko Afrika Kusini mwaka jana, ni kati ya mambo ambayo yametoa msukumo kwa uamuzi wake wa kuhamisha makazi.
Keko ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 25, tayari ameshaanza kazi ya kutengeneza rekodi akiwa chini ya usimamizi wa karibu kabisa wa lebo hii ambayo pia inafanya kazi na wasanii wa kimataifa kama vile Alicia Keys, Usher, Chris Brown na wengineo.
No comments:
Post a Comment