DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, November 19, 2013

Je Una Tiketi yako?


Katika kuelekiea show kubwa ya ya kihistoria katika tasnia ya burudani Tanzania ambapo wakali Peter na Paul Okoye, unawafahamu zaidi kama P Square watakuwepo Live wakifanya vitu vyao juu ya jukwaa katika viwanja ya Leaders Club Jumamosi hii, Zoezi la ununuaji wa tiketi linaendelea kwa kasi mtaani ambapo ticketi zinapatikana kwa bei ya shilingi 35,000 tu.

Kabla mwana hajawa si wako unaweza kuchapuka na kwenda kujipatia tiketi yako katika maeneo yafuyatayo; kwa wakazi wa Kinondoni Image View - Kibop Complex (Tegeta), Engen Petrol Station - Mbezi, Rainbow Social Club - Mbezi Beach, Puma Petrol Station - Mwenge, Samaki Samaki na Photo Point - Mlimani City, Hill Park Restaurant - UDSM, Zizzou Fashion - Sinza Afrika Sana, Big Bon Petrol Station & Super Market - Sinza Mori, Rose Garden - Mikocheni, Photo Point - Mayfari Plaza, Big Daddy - Facebook Take-Away (Morroco), Roby One Fashion - Kinondoni (Corner ya Mwananyama),  Best Bite - Namanga, Tasar Lounge - Coco Beach na Didis Bar - Oysterbay.

Kwa wale wa Ilala jichukulie tiketi yako sasa pale Steers - Mtaa wa Samora, Break-Point Bar - karibu na Bilicanas Club, Photo Point - Benjamin Mkapa Tower, Samaki Samaki - Samora Street/Avenue, Ambassador Lounge - Benjamin Mkapa Tower ama Photo Point pale Quality Centre.

Ukiwa Temeke unavuta tiketi zako za kutosha tu pale TCC CLub - Chang'ombe, Dar Live - Mbagala, . Mafuvu Baybeee Barber Shop - Mtoni, ama Kisuma (Old Sugar Ray) - Temeke.

Zingatia, Ni #PSquareLiveInDar November 23!!!, Hakosi mtu.

No comments: