
Mtandao maarufu unaosimamia kazi za wasanii nchini Kenya, umetoa orodha ya wasanii wa kike ambao kwa sasa ndio wanafanya poa na kuiendesha gemu ya muziki nchini humo ikiwa na majina ya wasanii kama Wangechi, Maia Von Lekow, Miss Karun pamoja na Atemi.
Madiva hawa wamekuwa na nyota ya kipekee katika muziki, hasa ukitazamwa uwezo wa Wangechi mwenye umri wa miaka 19 tu katika kuimba na kurap, Maia Von Lekow ambaye ameteka miondoko ya Jazz, funk, folk na blues, Miss Karun ambaye sauti yake imeweza kujipatia utambulisho wa kipekee katika muziki pamoja na Atemi ambaye ameibuka la ladha mpya ya muziki wa soul.
Mafanikio ya wanadada hawa hasa katika umri wao mdogo yametokana na kipaji kikubwa ambacho kimeweza kupata usimamizi na muongozo mzuri ambao umeweza kuwasaidia kuwa nyota zinazongara kutoka Afrika Mashariki, ambapo kwa sasa mwanga wake umeanza kuonekana sehemu mbalimbali za dunia.
No comments:
Post a Comment