
Wanandugu wawili ambao ni mapacha Peter Okoye na Paul Okoye, leo hii
wameushangaza ulimwengu mara baada ya picha zao wakiwa kwenye sebule na
dinning room iliyonakshiwa na dhahabu kwenye samani zake kuzagaa
mitandaoni huku zikisindikizwa na maneno yenye kujiamini ndani yake.


Maneno kama:-‘Goldenworld #blessed.’, ‘#2kings…… Work hard,play harder.’
na ‘A king in my own world…. #Blessed.’ yalitumika kusindikiza picha
hizo wakiwa kwenye pozi tofauti tofauti.


Kama kweli mng’o unaoonekana kwenye vitu hivi vyote ni dhahabu, basi
hakuna sababu kuna kila sababu ya kuwaita wafalme wa mziki Africa
kutokana na thamani ya pesa waliyotumia kutengeneza samani hizi.
No comments:
Post a Comment