Kufuatia tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya lililomkumba
msanii Bebe Cool wa Uganda mwaka 2010, msanii huyo amelipwa shilingi
milioni 380 za Uganda kwa maamuzi ya mahakama kuu, kama fidia ya
majeraha aliyoyapata na kusababisha kusitisha kazi zake za muda.
Bebe Cool anachukua mpunga huu japo kishingo upande, ambapo itakumbukwa kuwa kwa mujibu madai yake ya awali kabisa, msanii huyu alitaka kulipwa kiasi cha shilingi milioni 800 ambazo ndizo alizoona zinastahili kuziba hasara aliyotengeneza muda wote wa kuuguza majeraha yake.
Tukio hili la Bebe Cool kupigwa risasi mwaka 2010, linabaki kuwa moja ya matukio makubwa yaliyotikisa tasnia ya burudani nchini Uganda mpaka sasa, hasa ikizingatiwa kuwa askari polisi ndiye aliyekuwa mhusika aliyefanya tukio hili la kinyama.

No comments:
Post a Comment