DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, December 19, 2013

Nameless aahidi kitu mwaka mpya

 

 Nameless kutoka Kenya, baada ya ukimya wa kipindi kirefu sasa ametangaza kukusanya nguvu na kujipanga kwa ajili ya kuwapatia mashabiki wake ladha waliyoikosa kwa muda, kwa kuachia kazi yake siku ya Mwaka mpya.

Nameless ambaye kwa sasa pia ameonekana kuwa kikazi zaidi akitumia muda mwingi studio sambamba na kumsaidia Wahu kumtunza mtoto wao mchanga, amesema kuwa kazi hii mpya ni kutoka katika albam ambayo anashughulika kuikamilisha kwa sasa, albam ambayo pia itatoka mwaka kesho.

Ukimya wa Nameless umefanya mashabiki wa msanii huyu kusubiri kwa muda pamoja na kujiuliza maswali kibao ambayo yamepata majibu baada ya msanii huyu kutoa ahadi hii ya kufungua nao mwaka.

No comments: