DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, December 19, 2013

Belle 9 ajifua kwanza

 
Belle 9, moja kati ya wasanii wenye vipaji vikubwa kabisa vya kuimba hapa nchini Tanzania, ametolea ufafanuzi suala la albam yake ya Vitamin Music kutokuingia sokoni katika muda ambao alikuwa amewaahidi mashabiki wake, ambapo amesema kuwa suala hili limesababishwa na yeye kuwa kimya kwa muda.

Belle 9 ambaye sasa amejipanga kurudi kwa kasi katika chati za muziki kwa kuachia ngoma kadhaa, akiwa tayari ametanguliza ngoma ya 'Wanitamani' amesema kuwa, albam yake ipo na itatoka mara tu baada ya yeye kujirudisha katika chati.

Msanii huyu amekiri changamoto ya kuzidiwa na majukumu hasa kutokana na ukweli kuwa kwa sasa anafanya kazi yake akiwa hana msimamizi/meneja yoyote, huvyo kumfanya kuwa mtendaji mkuu katika shughuli zote zinazohusu muziki wake.

No comments: