DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, December 19, 2013

Niki wa Pilli ahimiza amani

 
 Msanii wa muziki wa Rap hapa Bongo, Nikki wa Pili amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Tanzania kutunza amani na utulivu iliyonayo kutokana na umuhimu wake mkubwa kwa jamii na maendeleo yake.

Rapa huyu ambaye ni mtaalam wa Maendeleo ya jamii amesema kuwa, kutokana na mifano halisi ya nchi jirani za DrR CONGO, Afrika ya Kati na Somalia ambazo wakazi wake wengi wamekumbana na mauaji ya kinyama, kuna haja kubwa ya Tanzania kujifunza na kuishikilia amani yake.

Ujumbe huu wa Nikki kuhusiana na amani kwa Mashabiki wake, unakuja wakati huu ambao ni msimu wa sikukuu pamoja na kufunga mwaka, ambapo ni muhimu sana kujiepusha na matukio ya uvunjfu wa amani na uhalifu ambayo hutokea mara nyingi.

No comments: