DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, December 19, 2013

Linah azungumzia mavazi yake

 
Msanii wa muziki Linah Sanga, ambaye kwa upande mwingine anasifika sana kwa kuvaa kimitego, ameweka wazi sababu ya yeye kuwa anavaa katika mtindo ambao umekuwa ukiwachengua sana mashabiki wake hususan wale wa jinsia ya kiume.

Linah katika mahojiano yake na eNewz ameeleza kwa kirefu kuwa mtindo wake wa mavazi umekuwa ukizingatia mazingira ambayo huwa anakuwepo, akishirikisha mawazo ya watu wake wa karibu juu ya namna ambavyo wanaona atapendeza na kuvutia watu zaidi akivaa.

Linah amesema kutokana na kuona dhahiri kuwa mavazi yake mara nyingi hususan katika maonyesho hayawafurahishi watu kadha wa kadha hususan wale waliokula chumvi nyingi kidogo, kwa sasa atakuwa akiliangalia swala hili na kushirikisha watu wengi ili kuhakikisha kuwa kile anachokivaa hakimletei madhara yanayoweza kumsababishia kupoteza mashabiki.

No comments: