DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, January 29, 2014

Bobi Wine kutoa vipaji Ghetto

 
Msanii wa muziki kutoka Uganda, Bobi Wine ametangaza kuendelea kwa mpango wake wa Ghetto Search For the Ghetto Superstar ambao unahusisha kusaka wasanii wenye vipaji kutoka katika jamii ya kawaida katika makazi yao sehemu mbalimbali huko nchini Uganda.

Mpango huu utakuwa unaendeshwa pia kupitia kipindi cha Televisheni cha maisha ya uhalisia cha msanii huyu ambacho kinakwenda kwa jina The Ghetto President ambacho awamu yake ya nne itaanza hivi karibuni huko huko Uganda.

Kwa upande mwingine, Bobi Wine pia kwa upande wa muziki wake ameanza vizuri mwaka kwa kuachia kazi inayokwenda kwa jina Dillema ambayo amemshirikisha Cindy pamoja na mkali kutoka Jamaica Mr G, kazi ambayo inatikisa chati mbali mbali za muziki nchini humo. 

No comments: