DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, January 29, 2014

Dimpoz ailaumu AM records

 
 Baada ya kuvuja kwa ngoma mpya kutoka kwa msanii Ommy Dimpoz, Miss Koikoi, ambayo yeye mwenyewe amesema imevuja na haikuwa katika mpango wa kutolewa, msanii huyu ametoa lawama zake kwa studio ya AM ambayo amesema ndipo aliporekodia kazi hii miaka iliyopita.

eNewz ilicheki na Ommy Dimpoz kuhusiana na tukio hili ambapo ametoa tamko lake rasmi kuwa ameshangazwa sana kuona kuwa kazi hiyo imeanza kusambaa mtandaoni bila yeye kuwa na taarifa yoyote, Ngoma ambayo aliirekodi miaka miwili iliyopita na kumweleza producer Manecky kuwa bado anaitaka kuirekebisha na kuiongezea vitu kabla ya kuitoa rasmi.

Ommy Dimpoz amesema kuwa yeye binafsi hana tatizo lolote na Maneck wala lebo ya AM Records ila atakaa na uongozi wake na kufanya maamuzi juu ya hatua atakayochukua dhidi ya record lebo hiyo kwa kuvujisha ngoma yake.

No comments: