DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, January 3, 2014

Dully kupewa shavu na mwanae

 
Msanii wa muziki Dully Sykes, amoenyesha jitihada za mapema za kumuingiza katika reli ya muziki mtoto wake wa kwanza ambaye anafahamika kwa jina Torry Sykes, ambapo hivi karibuni kwa mujibu wa Dully mwenyewe, msanii huyu kinda anatarajia kuachia ngoma yake akiwa amemshirikisha Dully mwenyewe ambaye ni mshua wake.

Dully Sykes amesema kuwa kazi hii itakuwa inasimama kwa jina Totoo na itatoka 'soon', na tayari mitaa imeanza kujawa na hamasa ya kujua ni nini baba na mtoto watakifanya katika colabo hii pamoja.

Dully Sykes ambaye anatamba sasa na ngoma yake ya Kabinti Special ndiye atakayehusika katika mpango mzima wa kutengeneza kazi hii safi.

No comments: