DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, January 30, 2014

Octopizzo awazodoa wenzake

 
Rapa Octopizzo wa nchini Kenya, ameripotiwa kutoa ya moyoni kuhusiana na wasanii wenzake ambao wanafanya muziki wa Injili hususan huko nchini Kenya, ambapo kwa mujibu wa mtazamo wake asilimia 70 ya wasanii hawa hufanya muziki huu kwa malengo ya kupata pesa zaidi.

Octopizzo amesema hadharani kuwa wasanii hawa wamegeuza lengo la muziki wa injili kutoka katika kusambaza ujumbe mzuri wa Mungu kwenda katika biashara, na hivyo kuondoa tofauti ya muziki wa injili na muziki wa ki-dunia.

Muziki wa injili nchini Kenya umekuwa na kujijengea nafasi kubwa katika soko la muziki nchini Kenya na Afrika Mashariki huku kukiwa na tofauti ndogo katika mtindo wa mavazi na dansi, kitu ambacho kimepelekea wengi kuwa na mtazamo wa tofauti juu ya muelekeo wa muziki huo.

No comments: