Msanii Habida kutoka nchini Kenya, ameweka wazi kuwa baada ya kusaini mkataba na lebo ya muziki ya Gallo Records ya huko Afrika Kusini, ratiba ya maisha yake imebadilika sana ambapo kwa sasa muda mwingi anakuwa huko Afrika Kusini kikazi.
Habida amesema kuwa muda mwingi amekua akiutumia kutengeneza rekodi mpya ambazo zitakuwa zinatoka kwa mipangilio kuanzia hivi karibuni.
Habida ambaye pia pembeni ya muziki anajishughulisha na masuala ya uigizaji, pia anatarajia kuendelea kushine kupitia vituo vikubwa vya Televisheni Afrika kupitia ushiriki wake katika project kadhaa kubwa za maigizo huko Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment