DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, April 9, 2014

MZEE YUSSUF ALAANI KUPAKAZIWA UONGO MTANDAONI

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Ni kiongozi wa Jahazi, Mzee Yussuf aka ‘Mfalme’anayefanya vizuri kwenye game la muziki wa Taarabu Nchini.

Amefunguka na kuwazungumzia watu wanao fungua facebook kwa kutumia majina ya Mastaa kwa lengo la kuwapakazia habari zisizo za ukweli alizungumza kauli hii baada ya kumvutia waya kwenye simu ya mkononi kuhusiana na habari iliopostiwa jana na jamaa anaye tumia jina hili.
Mzee Yusuph Fake;” Habari za usiku huu,Napenda kuwataarifu wapenzi wangu wa Muziki wa Taarabu Albamu yangu ya CHOZI LA MAMA ndio Albamu yangu ya mwisho.Natarajia kuacha muziki mwishoni mwa mwaka huu,kuna vitu vingi vya kufanya Sitaki kuzeeka kwenye Muziki.Kuna vitu vingi vya kufanya kama kuuza Duka n.k.Na hata nikigombea Ubunge si Mtanipa?????!!!!!”
Mzee Yussuf Orginal “Kiukweli habari hii si ya ukweli huyo ni jamaa anaye tumia jina langu kupost vitu vya uongo na sio yeyetu wapowengi tena wengine ni marafiki zangu nikiwagundua tu wana ni block mimi sija post kitu kama hicho hata jina nalotunmia facebook ni ‘Mzee Yussuf. Nilisema Chozi la mama itakuwa Album yangu ya mwisho kwa mwaka huu sio kwamba naacha kuimba huo ni uongo”

No comments: