Baada ya kushinda tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki kutoka katika
tuzo kubwa za muziki za KTMA, Jose Chameleone ambaye amekuwa Tanzania
kwa siku kadhaa sasa, amekimwagia Kiswahili, lugha ambayo imemfanya
kueleweka Afrika Mashariki.
Chameleone
ambaye ameshinda tuzo hiyo kupitia ngoma yake ya Tubonge, amefanikiwa
kujizolea mashabiki mbalimbali kutoka nchi hizi za Afrika Mashariki
kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba katika lugha ya Kiingereza,
Kiswahili na Kiganda.
Msanii huyu amesema pia kuwa anashukuru sana kwa kuweza kushinda tuzo
hii mfululizo kutokea mwaka 2012, dalili inayyonyesha kuwa Afrika
Mashariki inafurahia kazi zake anazozifanya kwaajili ya kuwaburudisha.
No comments:
Post a Comment