DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, March 27, 2014

Bob Junior awashangaa BASATA kwa walichokifanya kwa Snura, Madee na Jux

5e5dd8e6a59f11e3a8080e78bfefbac0_8 


Wasanii mbalimbali wameendelea kuulalamikia uamuzi wa BASATA wa kuwafungia Snura, Jux na Madee kushiriki katika tuzo za KTMA kwa kile kinachosemsekana Video zao kukinzana na maadili ya KiTanzania. Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram Bob Junior ameamua kufunguka kuhusiana na swala hilo.
Bob Junior aliandika “SIJAONA HAKI/SABABU YA HIZI NYIMBO KUONDOLEWA NA BASATA @juma_jux #uzuri wako @snuramushi #nimevurugwa @madeeali #temamate Wasanii ndo tunatunga nyimbo ziendanazo na globallaization kwan vijana wanapenda kutuona tofauti kama niivyo wawe wana tutungia wenyewe nyimbo kwasababu wanao chambua nyimbo ni wazee wanachotaka nass tuwe wazee” 
Siku ya juzi ikiwa ni masaa machache tu baada ya uamuzi huo kutangazwa na BASATA Diamond alifunguka na kusema  Ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje, kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake Haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje… Hii ni sawa na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu… Will the target of reaching our goals ever be achieved?? #Ni_Mtazamo_tu.”

 69d5fdaab5aa11e38753125b8789c25f_8

No comments: