Yakiwa yamepita masaa machache tu tangu Basata watangaze majina yatayowania Tuzo za KTMA 2014. Diamond ameamua kufunguka na kulaani
kitendo kilichofanywa na Basata cha kuwafungia Jux, Madee na Snura
kutokana tu na video zao kuonekana hazikizi maadali ya Kitanzania.
Kupitia akaunti yake ya InstagramDiamond aliandika “Ikiwa kweli
tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa,
nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje, kuliko
kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake Haufikii hata
robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje… Hii ni sawa
na kuzidi kuukuza mziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu…
Will the target of reaching our goals ever be achieved??
#Ni_Mtazamo_tu.”
Fans wa Diamond Instagram nao hawakuakaa kimya na kuamua kumuunga mkono Diamond, na hizi ni baadhi ya maoni waliyotoa.
minaemmy Yaaan nachokiona mm naona wanataka kuua kizazi hiki cha mziki na cio fresh mm cio msaani ila imeniuma kweli!
marwamnanka Ukiona mtoto wako anaharibika na
anaemuharibu ni wa jirani anza kwaza kumzuia wa jirani acje nyumbani
then ndo umzuie na wa kwako
ashurayusuph Kweli kabisaaa wala hujakosea wenzetu
hata uchi wanacheza muziki au filam tunaletewa na tunaangalia wala
hazifungiwi kunya anye kuku akinya bata et kaarisha
No comments:
Post a Comment