Msanii wa muziki Lameck Ditto, ametoa ushauri wa bure kwa wasanii
wenzake kujaribu kuangalia namna ambavyo wanaweza kutumia vipato
wanavyotengeneza katika muziki, kuwekeza katika miradi na shughuli
mbalimbali, na kuacha kuendekeza starehe.
Ditto
amesema kuwa, kwa hulka yake binafsi anaona kuwa kuna umuhimu mkubwa wa
kuwekeza na kuongeza njia za vipato, ambapo yeye binafsi amekwishaanza
kuonyesha mfano kwa kujishughulisha na kilimo pamoja na shughuli
nyingine ambazo zinamsaidia kuendesha maisha yake vizuri.
Huyu hapa Ditto mwenyewe akimwaga somo hili kali kwa wenzake;
No comments:
Post a Comment