Msanii Kenzo kutoka nchini Kenya, baada ya kutangaza kuwa mambo yake
sasa yameanza kumnyookea baada ya kutoka chini ya usimamizi ya lebo ya
Ogopa, ameweka wazi kuwa kwa sasa yupo katika hatua za mwisho za
makubaliano kuingia katika mkataba huo.
Kenzo
amesema kuwa, katika mkataba huu mpya atakaoingia, atakuwa na uhuru wa
kurekodi kazi zake sehemu nyingine yoyote ile, tofauti na mkataba wa
awali ambao ulikuwa ukimbana kufanya kazi sehemu moja.
Endapo mipango hii ya Kenzo itanyooka kama matarajio yake yalivyo,
itakuwa ni nafasi nyingine kubwa ya msanii huyu kuweza kufanikiwa
kuingia kwa nguvu katika soko la muziki la Kimataifa.
No comments:
Post a Comment