DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, July 8, 2014

IZZO BIZNECC KUACHIA NGOMA WIKI HII

izzo1 


Msanii Mkali anayewakilisha Mbeya City Izzo Bizness anatarajia kuachia ngoma This Week, Hapa Izzo anafunguka zaidi……
”Ni bonge la Ngoma ambayo ni kali sana ndani yake nimezungumzia walalahoi wenzangu; Hope Mashabiki wangu wataipenda na itakuwa Gumzo kitaa kwa sana coz inaelezea maisha ya watu wa kawaida sana, so Wiki hii ndo natarajia kuachia na kuitambulisha Rasmi, naomba Mashabiki wangu popote walipo waipokee kwa Mikono miwili coz mimi nakuja tofauti kidogo safari hii,ntagusa kila kona katika jamiin si zungumzii Mapenzi tu bali nagusa kila Kona na ninapenda kubadilika.


BOB JUNIOR ATOA RED CARD KWA MKEWE

Mke wa Bob Junior 

Hit maker wa ngoma ya ‘Bashasha’ Raheem Rummy Nanji aka Bob Junior baada ya kurudiana na mkewe Halima Ally miezi kadhaa iliyopita kutokana na ndoa yao kuvunjika kwa sababu ya Bob Junior ku-cheat nje ndoa na kufumaniwa na vic***.
Kwa sasa mkali huyo ametoa tena talaka 3 kwa mkewe Halima kutokana na tetesi zilizopo chini ya
carpet kuwa ndugu wa Bob Junior wanamuona Halima aka mama Rummy hana nyota angavu kwa mumewe kitu kinachosababisha Bob kufifia katika ramani ya kimuziki, BK Cop alivyozinyaka info’s akamvutia waya Bob Junior ili kuhakikisha ni kweli red card imetolewa tena?
BK: Mambo vipi Bob Junior?
BOB JUNIOR: Poa niaje man.
BK: Poa, nasikia umempiga chini mkeo?
BOB JUNIOR: Mimi nilikuambia sijawahi kurudiana naye tangu tulivyoachana mwanzo.
Ingawa wanamwagana ila wamebahatika kupata mtoto mmoja ‘Rummy’ mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kadhaa hadi sasa.



Sunday, July 6, 2014

Diamond Platnumz atinga ndani ya studio za Genn Online Radio

Diamond Platnumz alipokuwa akiwasili kwenye mji wa Olathe jimbo la Kansas ilipo Radio hiyo ya GENN kwa mahajiano kabla ya show yake inayotarajiwa kufanyika muda si mrefu katika anuani ya 8625 Troost Ave, Kansas City, Missouri.


IMG 1642 Mtangazaji wa GENN Radio AJ (mwenye kofia nyeusi wapili toka kulia) akimfanyia mahojiano Diamond Platnumz ndani ya Studio ya Radio hiyo ambayo inapatikana mtandaoni www.gennmedia.com wengine ni Dj Romy Jons Poromota DMK na Dj Boston (kulia).

IMG 1644 
 Dj Boston na AJ wakimsikiliza Diamond Platnumz wakati akijibu moja ya maswali waliyomuuliza.


IMG 1646 
 Mashabiki wakiwa ndani ya studio za GENN Radio wakimsikiliza Rais wa Wasafi akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na AJ.


IMG 1650

 Diamond Platnumz akiendelea kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na AJ huku Dj Romy Jons akifuatilia kwa makini maswali na majibu yaliyokua yakiulizwa AJ na kujibiwa na Diamond Platnumz.



Sunday, June 1, 2014

MNYAMA HATOSAHAU LUPANGO


Mnyama TID amesema kitu ambacho hawezi kukisahau katika maisha yake ni kwenda jela.
“In fact time ambayo nilipata fight nikaenda jela, I was down ,nimeenda jela , so it’s like falling down,” alikiambia kipindi cha XXL.
“Nilivyokuwa nimekaa kula jela and love ambayo nimepata kutoka kwa watu wa mule ndani lakini nimetoka mpaka leo am still shining, lakini ili ilikuwa down fall, Mungu amepanga this guy is an artist, tumembless afanye muziki, inspiration yangu ni kubwa sana, wasanii wengi ambao wamefanya kazi na mimi wamepata hata mafanikio in one way or another kabisa.”


Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema anatarajia kuachia album iitwayo ‘Chumvini’.

 
 “Plan yangu hivi sasa tunatoa album ya Chumvini ,pia tunamaliza kushoot filamu, tumeanza kushoot baadhi ya scene ili tuzipresent kwa sponsor, we have a teaser, lakini tutaendelea kufanya vitu ambavyo tunatakiwa kufanya. Nashukuru ,ungu Jay Mo in the plan , na Jay Mo ni actor mzuri sana he is a comedian.”




SHILOLE AKAE CHONJO NA SIFA ZA MASHABIKI

 Shilole ft.Rich Mavoko_ kitokololo - viuno tucheze_11

Msanii wa muziki wa Mduara Tzee Zuwena Mohamed
aka Shilole aka ‘Shishi Baby
‘ ni Mdada anaye jituma sana kwenye Muziki wake,kwa kuimba vizuri,kutenda haki akiwa kwenye stage.
Mbali na kuwa katika level nzuri alionayo kupitia jasho lake kwa Muziki, pia mashabiki wamemtaka ‘Shishi’ kuto lizikika na misifa wanayo mwagia kila wakati kwa madai ya kuwa juhudi za shilole zinawatia moyo fans,
Hata hivyo baadhi ya mashaiki wake wamesema kuwa “Sifa zikimpa kiwewe shilole, inaweza kuwa ndio mwanzo wa kushuka, kimuziki hivyo juhudi zaidi ndio kitu fans wake tunakitaka”.

DIAMOND AKILA BATA NA MASHBIKI WAKE WASHINGTON DC

 

 Diamond Plutnumz akiongozana na wasafi pamoja na Dj Romy Jons (Dj wake) kulia wakiwa na mwenyeji wao DMK wakiwasili tayari kukutana na mashabiki wake waliofika kwenye mgahawa wa Safari, Washington, DC kumsubili na kupiga nae picha.


Tuesday, May 6, 2014

Nikki Mbishi apania kubadili mtazamo

 

 Mkali wa michano ambaye anafanya poa hapa Tanzania, Nikki Mbishi a.k.a Nikki Zohan, ambaye katikati ya mwaka huu anatarajia kuachia albam yake mpya 'Ufunuo', amesema, hatua yake ya kuachia albam hii ni kipimo cha ukubwa wa uwezo wake katika rap.



Nikki Mbishi amesema haya kutokana na imani inayoendelea sasa kwa wasanii na wadau wa muziki kuwa biashara ya albam za muziki hususan wa Bongoflava na Hip Hop hailipi, na kuhusiana na hili, hapa anaelezea juu ya alivyojipanga na albam hii.
Msanii Nikki Mbishi amesema kuwa, wasani wengi hapa nchini wanaogopa kutoa albam kwasababu ya kutokuamini uzuri wa kazi zao, na pia kutokana na kutokupenda kazi zao tofauti na yeye ambaye anaajiamini na kuamini kuwa kazi yake ni nzuri na ni biashara tosha.

Nonini kutoka misaada kupitia Michezo

 

 Msanii wa muziki wa Genge kutoka nchini Kenya, Nonini pamoja na marafiki zake wameibuka na njia mpya ya kuchangisha pesa kwaajili ya shughuli za hisani, na hii ni kupitia mashindano ya wa mpira wa kikapu ambao huzikutanisha timu mbali.


Mashindano haya ya mpira wa kikapu yamepatiwa jina (Entertainment With Fun 4 Charity), ambapo kwa mujibu wa Nonini, yatakuwa yakifanyika kila sikukuu, huku wakiwa wamepanga kukutana tarehe 1 mwezi June tena kwaajili ya mechi nyingine kali.
Katika mashindano ya kwanza yaliyofanyika, kiasi cha shilingi za Kenya 120000 zilipatikana, ambapo asilimia 50 ya pesa hizi ilipelekwa katika kituo cha kulelea watoto cha Filomena kilichopo huko Kayole.


Chameleone akimwagia sifa Kiswahili

 

 Baada ya kushinda tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki kutoka katika tuzo kubwa za muziki za KTMA, Jose Chameleone ambaye amekuwa Tanzania kwa siku kadhaa sasa, amekimwagia Kiswahili, lugha ambayo imemfanya kueleweka Afrika Mashariki.


Chameleone ambaye ameshinda tuzo hiyo kupitia ngoma yake ya Tubonge, amefanikiwa kujizolea mashabiki mbalimbali kutoka nchi hizi za Afrika Mashariki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba katika lugha ya Kiingereza, Kiswahili na Kiganda.
Msanii huyu amesema pia kuwa anashukuru sana kwa kuweza kushinda tuzo hii mfululizo kutokea mwaka 2012, dalili inayyonyesha kuwa Afrika Mashariki inafurahia kazi zake anazozifanya kwaajili ya kuwaburudisha.

Man Water amjibu Sheddy, atetea ushindi

 

 Mtayarishaji wa Muziki wa kizazi kipya Man Walter ameamua kufunguka juu ya tuzo aliyopata kutokana na maneno ya mtayarishaji mwenzake Sheddy Clever, na kusema kuwa alistahili kupata tuzo hiyo


Baada ya mtayarishaji muziki Sheddy Clever kulalamika kukosa tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya huku kazi aliyotengeneza ikichukua tuzo ya wimbo bora wa kizazi kipya wa mwaka, na kutoa kauli kuwa hata Man Water ambaye ndiyo ameshinda tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Muziki wa kizazi kipya kwa mwaka huu anafahamu kuwa hakuwa ana stahili tuzo hii, Man Water mwenyewe ameamua kufunguka juu ya maneno ya Sheddy Clever.
Mtayarishaji muziki huyu kutoka Combinations Sound amesema kuwa, kushinda kwake tuzo hii licha ya kuchangiwa na mashabiki pia kunatokana na kazi zake kufanya vizuri, na hapa anaeleza zaidi juu ya kauli aliyoitoa Sheddy Clever dhidi yake.

 

Sunday, May 4, 2014

Historia Concert kufanyika tena karibuni

 
Onesho la Historia la mwanadada Lady Jay Dee, limesogezwa mbele baada ya hali ya hewa ya mvua kuzuia mashabiki waliohudhuria Tranic Plaza, Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam usiku wa jana, kupata burudani kikamilifu zaidi.
 
Katika onesho hili, ili kuwapa ladha wapenzi na mashabiki wa mwanadada Lady jay Dee waliohuduria, wasanii Dabo, Patricia Hillary, Roma Mkatoliki na Baghdad, Professa Jay na pia Machozi Band ikiongozwa na Lady Jay Dee walipanda jukwaani kutumbuiza kidogo.
Baada ya tukio hilo, eNewz tukaongea na Lady Jay Dee ambaye alizungumzia show hii, na kutangaza zawadi ya show nyingine kali ya Historia hivi karibuni katika mazingira ambayo yataruhusu watu kujiachia kufurahia burudani zaidi.

 

'Jasho' la Barnaba Classic kutikisa kideoni

 
Jasho La Mnyonge, ngoma ya msanii Barbaba Classic ambayo video yake imekuwa ikisubiriwa kwa hamu kwa muda sasa hatimae imetoka, ambapo msanii huyu ameahidi tukio kubwa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa kazi hii hivi karibuni.
 
Kazi hii safi ambayo imeongozwa na mtayarishaji video Saidi Hamadi, tayari imeanza kupokelewa vizuri miongoni mwa mashabiki wa msanii huyu kwa njia ya mtandao na vituo mbalimbali vya televisheni.
 
 

Jaguar arudisha shukrani kwa Wafungwa

 
Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Jaguar kwa jina maarufu, kwa mara nyingine ameonyesha moyo wake upendo kwa kuamua kurudisha shukurani katika gereza la Industrial Area huko Kenya, mahali ambapo alifanya sehemu ya video ya ngoma yake ya 'kioo'.
 
 
Jaguar katika ziara yake hii gerezani, mbali na kuwashukuru wafungwa na maafisa gereza kwa ushirikiano, pia aliwabebea zawadi mbalimbali kwaajili ya kuwapatia na wao nafasi ya kufurahi katika kipindi cha sikukuu iliyomalizika ya Pasaka.
Katika ziara hii ya Jaguar ambayo imesukumwa kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya Video yake ya Kioo, Jaguar pia ameripotiwa kuahidi kumsaidia kwa nguvu zake zote moja ya mfungwa ambaye ameonyesha kipaji cha kuimba cha aina yake.

Weasel, Pallaso, AK47, Chameleone waingia vitani

Wasanii wa muziki kutoka familia moja huko nchini Uganda, Weasel, Pallaso, AK 47 pamoja na Jose Chameleone, wameendelea kutumia vipaji vyao vikubwa katika kuleta ladha na ushindani katika muziki wa Uganda.
 
Chameleone, Weasel, Pallaso, AK47
Wasanii hawa kwa ujumla wao wameamua kutengeneza makundi mawili na kufanya rekodi ambazo mashabiki wataamua mkali aliyemfunika mwenzake.
Ndugu hawa katika mpango huu wamejigawa ambapo Chameleone amefanya kazi inayokwenda kwa jina Kaleeba akiwa na mdogo wake wa mwisho AK47, huku Weasel pamoja na Pallaso wakitengeneza timu yao na kutoka na rekodi ambayo inakwenda kwa jina Omugongo, rekodi zote hizi zikiwa zimefanya na mtayarishaji mziki mmoja.
Kwa njia ya mtandao, Pallaso ambaye kazi zake nyingi anafanyia huko Marekani, amewataka watu kusikiliza rekodi hizi kali na kuamua ni kundi gani limemfunika mwenzake kutoka familia yao hii ya kimuziki ya wana-Mayanja.

Afande Sele kuuenzi Ufalme wa Rhymes

 
Msanii wa muziki Afande Sele kutoka pande za Morogoro, katika kuenzi ukongwe wake katika game ya muziki, ameamua kuenzi heshima na taji lake la Mfalme Wa Rhymes Tanzania.
 
 
Itakumbukwa kuwa, heshima hii ya Ufalme wa Rhymes alipatiwa Afande Sele miaka 10 iliyopita katika mashindano ambayo hayakuwahi kuendelea tena, hivyo ameamua kufanya tukio kubwa la kuadhimisha kudumu kwa taji hilo mikononi mwake pamoja na heshima hii bila kupata mrithi ama mpinzani kwa muda wote huu.
Afande amesema kuwa, kwa sasa yupo katika hatua za maandalizi ya tukio hili kubwa ambapo atatumia muda wake mwingi jijini Dar es Salaam kuanzia sasa, ili kuhakikisha kuwa anaweka kila kitu katika mstari kwaajli ya maadhimisho haya ambayo yatafanyika mjini Morogoro.
Msikilize mwenyewe akifunguka zaidi hapa......
 
 

Size 8 kung'ara tuzo za Groove

 
Wasanii wanaowania tuzo za muziki wa Injili za Groove za huko nchini Kenya kwa mwaka 2014, wametangazwa majina yao, ambapo katika orodha hii msanii Size 8 kati ya wengine ameweza kungara kwa kutokea katika vipengele vitatu muhimu.
 
Kwa mujibu wa orodha hii, Size 8 akikabiliwa na wasanii wakali katika upande wa muziki wa injili ambao ameanza kuufanya muda si mrefu, anatokea katika kipengele cha Msanii bora wa kike wa mwaka, Wimbo bora wa mwaka na video bora wa mwaka kupitia rekodi yake ya Mateke.
Katika tuzo hizi, wasanii wengine wakali pia kama Jimmy Gait, Rufftone na Daddy Owen pia wanaingia katika baadhi ya vipengele na kufanya msisimko mkubwa kuelekea kuwatambua washindi halisi pale tuzo hizi zitakapotolewa, tarehe 3 mwezi Juni.

 

Snura aweka mambo sawa

 
 
Msanii wa muziki Snura, ambaye umaarufu wake ulianzia katika sanaa ya maigizo, amekanusha taarifa za yeye kujiingiza katika muziki kwa nia ya kuwapiga madongo mahasimu wake.
 
Snura amesema kuwa, kuingia kwake katika muziki ni kutokana na uwezo wake katika sanaa, na pia muziki wake ni kwa ajili ya kutoa ujumbe kwa jamii na pia kuburudisha, tofauti kabisa na nia ya kutupia watu madongo kama ambavyo watu wengi wanavyokuwa wanatafsiri.
Tumeongea na Snura kuhusiana na ishu hii, na hapa mwenyewe anaweka mambo sawa sawa.

Peter: Ni kweli kulikuwa kuna ugomvi kati yetu

 
Siku kadhaa baada ya taarifa juu ya ugomvi ndani ya kundi la P Square, ambao ulizua hofu ya kuvunjika kwake likiwa katika kilele cha mafanikio, Moja ya wasanii kutoka kundi hili, Peter Okoye amekiri kuwa ni kweli kulikuwa na ugomvi kati yao.
 
Peter, Paul na familia
Peter amesema kuwa, ugomvi ulioibuka kati yao ni kama ambavyo inaweza kutokea kwa watu wengine wowote ambao ni ndugu, na sasa umekwisha, ingawa hakutaja sababu rasmi za kutokea kwa ugomvi huu uliofanikiwa kuviteka vichwa mbalimbali vya habari vilivyo.
Ugomvi huu pia umehusishwa na mpango wa wasanii hawa kujaribu kutafuta kiki ya kutangaza ujio wa albam yao mpya, katika wakati huu ambapo wamekuwa katika mishe za kutengeneza video ya ngoma ya Testimony nchini Afrika Kusini.



 

DIAMOND AFUNIKA BOVU KTMA 2014

image
 
Diamond Platnumz amethibitisha kuwa ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya usiku wa Jumamosi kunyakua vipengele vyote zote saba alivyokuwa ametajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA.
Ommy Dimpoz akiongea kwa niaba ya Diamond Platnumz
Muimbaji huyo aliyekuwa ameambatana na mchumba wake Wema Sepetu amechukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, wimbo bora wa afro pop na video bora ya mwaka kwa wimbo wake ‘My Number On’e pamoja na Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki na Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) akimkabidhi tuzo Diamond, kushoto ni producer wa My Number One, Sheddy Clever

 
 
 





Mtangazaji wa Clouds FM, Adam Mchomvu akimkabidhi Fid Q tuzo
Nalo kundi la Weusi limeibuka na tuzo mbili, Wimbo bora wa Hip Hop (Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako) na Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya.
Weusi wakipokea tuzo
Vanessa Mdee akimbusu Lulu baada ya kukabidhiwa tuzo ya wimbo bora wa R&B
Jose Chameleone akipokea tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki
Wasanii wa Kenya, Amani na Wyre wakimkabidhi tuzo Luiza Mbutu
Isha Ramadhan akipokea tuzo
Wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Mwana FA, Weusi, Madee, Vanessa Mdee, Meninah, Angel, Makomando, Msami, Twanga Pepeta, Extra Bongo na wengine.
Tazama orodha nzima ya washindi wa tuzo hizo.

 

DIAMOND PLATNUMZ AVUNJA RECORD

e0a8228fb8L
 
Katika tuzo za kili Music Awards zinazofanyika kila mwaka hapa Bongo na kudhaminiwa na kinywaji cha bia ya Kilimanjaro, siku ya jana katika ukumbi wa Mlimani City kulikuwa na shangwe za kufa mtu baada ya mkali kutoka Wasafi Classic ‘Diamond Platnumz’ kunyakuwa tuzo saba zilizoshindanishwa katika vipengele tofauti tofauti, kwa ushujaa huo amevunja record iliyowekwa na msanii Twenty Percent ambaye awali aliwahi kuchukua tuzo tano kwa mpigo sasa kwa Diamond Platnumz jana ameweza kujinyakulia tuzo saba za ‘Wimbo bora wa mwaka’, Mwimbaji bora wa kiume, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki, Mtunzi bora wa mwaka kizazi kipya, Video bora ya muziki ya mwaka, Wimbo bora wa Afro Pop, Wimbo bora wa kushirikiana.
Huyu ndiyo Mr. Ngololo na tuendelee kutompigia kura katika tuzo ya MTV ili akamilishe ndoto yake.
 
 

“KILI MUSIC AWARDS WAMEFANYA KWELI”

_MG_0527
 
Msanii wa Hip Hop Farid Kubanda aka Fid Q baada ya kusotea sana tuzo za kili Music kwa muda mrefu bila kukata tamaa, siku ya jana kwenye tuzo hizo zinazofanyika kila mwaka ameweza kujinyakulia tuzo mbili kama ‘mtunzi bora wa Hip Hop na Msanii bora wa Hip Hop 2014, lakini Fid Q baada ya kuchukua tuzo hizo alifunguka na kusema “Kili Music Awards kwa sasa mmefanya kweli na washukuru sana asanteni sana.”
 
 

NIKKI MBISHI- UTAMWAMBIA NINI


SUNDAY FLEVA NA DJ BOSTON





Usikose kutegea sikio kipindi chako cha SUNDAY FLEVA toka GENN RADIO leo saa nane mchana kwa saa za marekani ya kati ,saa mbili usiku kwa saa za uingereza na saa nne usiku kwa saa za afrika mashariki kusikiliza kutoka kwenye simu yako bonyeza hapa: http://www.liveradio.gennmedia.com/live.mp3   na  kuangalia live bonyeza hapa: http://www.gennmedia.com/index.php/live-stream-top

Saturday, May 3, 2014

P Square mambo shwari sasa

 
Baada ya tetesi za kutokea mpasuko ndani ya kundi la P Square kuchukua nafasi kwa siku kadhaa sasa, taarifa mpya inayoashiria kuwa kwa sasa mambo yapo shwari kati ya Peter na Paul imeibuka hasa baada ya wawili hawa kuonekana hadharani kwa pamoja.
 
Hii inakuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Peter na Paul kuonekana hadharani baada ya ugomvi kati yao kuripotiwa na kuzua wasi wasi mkubwa kwa mashabiki wa kundi hili juu ya kutengana kwao wakati wakiwa katika kilele cha mafanikio.
Chanzo cha taarifa za kuwepo kwa ugomvi katika kundi hili kilikuwa ni ujumbe wa meneja na kaka wa damu wa wasanii hawa, Jude Okoye kutangaza mtandaoni kuwa baada ya miaka mingi ya mafanikio anaona kuwa sasa imetosha.

Friday, May 2, 2014

Ulokole wamshinda Bamboo

 
Rapa Bamboo ameibuka na jambo jingine jipya ambalo limeanza kuzua maswali juu ya uhalali wa maamuzi yake ya kutangaza kuokoka na kuachana na muziki wa dunia, na hii ni baada ya kuachiwa kwa kazi mpya yenye mrengo wa kidunia.
 
Kazi hii inayokwenda kwa jina Like it or Not, Bamboo ambaye kuokoka kwake kumeenda sambamba na kujibadilisha jina na kujiita Abraham, alitangaza pia mpango wake wa kuwa anafanya ngoma za kueneza ujumbe wa Mungu tu, na kupitia kazi hii mpya anaonekana na wasanii Guru Gang pamoja na Sharama wakiwakilisha yale yale aliyotangaza kuachana nayo.
Mpaka sasa bado hakuna ufafanuzi wowote kutoka kwa Bamboo kuhusiana na hiki kinachoendelea sasa katika kazi zake ikihusianishwa na msimamo wake wa kiimani ambao anaufuata sasa.