Baraza la sanaa la Taifa (BASATA)Leo
limetangaza rasmi matokeo ya mchakato mzima wa kuwapata wateule rasmi
wa vipengele 34 vya Tuzo za muziki Tanzania.Akiongea na
waandishi wa habari Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA,Godfrey .L.Mngeleza
alisema , zaidi ya mapendekezo 30,000 yalitumwa kwa njia ya sms na
mtandaoni.Hata hivyo alidai kuwa nyimbo ‘Uzuri wako’ ya
jux,’nimevurugwa’ ya Snura na ‘tema mate tuwachape’ ya Madee
zimeondolewa katika mchakato huo kwa madai kuwa zimevunja maadili na
hazifai kwa jamii ya Tanzania.
Nyingine ni
WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI – Tubonge ya Jose Chameleone, Nakupenda
pia ya Wyre na Alaine, Badilisha ya Jose Chameleone, Kipepeo ya Jaguar,
Kiboko changu ya Amani, Weasal na Radio.
WIMBO BORA WA TAARAB – Wasiwasi wako wa Mzee Yusufu, asie kujua
hakuthamini Isha na Saida Ramadhani, Nipe stara Rahima Machupa, sitaki
shari Leila Rashid, fahari ya mwanamke ya Khadija Kopa, mambo bado
Khadija Yusufu, kila muomba Mungu ya Mwanahawa Ally.
WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL – Nishai ya Chibwa ft Juru, Sexy Lady ya
Dr. Jahson, My sweet ya Jettyman Dizano, feel alright ya Lucky Stone na
wine ya Princess Delyla.
WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHWA/KUSHIRIKIANA – Muziki gani ya Ney wa Mitego
ft Diamond, Joto hasira ya Lady Jaydee ft Prof J, kidela ya Ally Kiba na
Abdu Kiba, bila kukunja goti ya MwanaFA, Ay ft J Martins na tupogo ya
Ommy Dimpoz ft J Martins.
RAPA BORA WA MWAKA WA BENDI – Kitokololo, Chokoraa, Ferguson, Canal Top na Totoo ze bingwa.
MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI – Khadija kopa, Vanessa Mdee, Isha Ramadhani, Luiza Mbutu, Catherine (Cindy)
MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA TAARAB – Enrico, Ababuu mwana wa Zanzibar na Bakunde.
MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA (BENDI) – Allan Mapigo, C9, Enrico, Amoroso na Ababuu mwana wa Zanzibar.
WIMBO BORA WA REGGAE – Niwe nawe ya Dabo, hakuna matata ya Lonka, tell
me ya Dj Aron ft Fidempha, bado nahitaji ya Chikaka ft Bless P &
Lazzy B, Bongo reggae ya Warriors from the east.
WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA KITANZANIA – Kwejaga nyangisha ya
Batarokota, Nalonji ya Kumpeneka, bora mchawi Dar bongo massive, tumbo
lamsokota ya Ashimba, Aliponji ya Wanakijiji na Agwemwana ya Cocodo
african music band.
Credit : Millard Ayo